Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Mahmoud Rajabi, mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza nchini Iran, na mjumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Wataalamu wa Uongozi, katika barua aliyomwandikia Papa Leon wa Kumi na Nne alimshukuru kwa msimamo wake wa kulaani mauaji ya watoto, wanawake na wanaume wasio na hatia na waliodhulumiwa.
Rais wa Taasisi ya Elimu na Utafiti ya Imam Khomeini (rh), huku akilaani matusi ya Trump mhalifu dhidi ya kiongozi wa Wakristo duniani, alionya kwamba; iwapo wafuasi wa Nabii Isa (as) na dini zote za Ibrahimu hawatasimama dhidi ya kiburi, udikteta na majivuno ya Firauni wa zama hizi, basi wanapaswa kutarajia matusi na hatari zaidi.
Matini kamili ya barua ya Ayatullah Rajabi ni kama ifuatavyo:
بسم الله الرحمن الرحیم
إِذْ قالَتِ الْمَلائِکَةُ یا مَرْیَمُ إِنَّ اللَّـهَ یُبَشِّرُکِ بِکَلِمَةٍ مِنْهُ اسْمُهُ الْمَسِیحُ عِیسَی ابْنُ مَرْیَمَ وَجِیهاً فِی الدُّنْیا وَ الْآخِرَةِ وَ مِنَ الْمُقَرَّبِینَ
Mheshimiwa Papa Leon wa Kumi na Nne
Kwanza kabisa, napenda kutoa shukrani na kuthamini kauli zako zenye thamani katika kulaani mauaji ya watoto, wanawake na wanaume wasio na hatia na waliodhulumiwa. Hatua hii iko katika mwelekeo wa mafundisho ya Kiungu ya Nabii mkubwa wa dini ya Ibrahimu, Nabii Isa Masih (as).
Kama unavyojua, Qur’ani Tukufu katika aya nyingi imemsifu Nabii Isa Masih (as), mama yake mtakatifu Bibi Maryam (sa), pamoja na wafuasi wake wa kweli na mitume wake waaminifu.
Sisi nchini Iran tumekuwa tukiishi kwa miaka mingi kwa utulivu na mshikamano pamoja na Wakristo wengi wapendwa, na bado tunaendelea hivyo.
Kiongozi shahidi na mtukufu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah al-Udhma shahidi Sayyid Ali Husseini Khamenei (qaddasallahu nafsahu al-zakiyyah), kwa miaka mingi, katika siku za Krismasi alikuwa akitembelea familia za mashahidi Wakristo na kukutana nao, na kuwafariji moja kwa moja. Yeye alikuwa kama baba mwenye huruma kwa watu wote wa Iran, wakiwemo wafuasi wa Nabii Isa (as), na hasa familia za mashahidi Wakristo.
Rais wa Marekani anayechukiwa, mbali na kuwaua wanawake, watoto na wanaume wasio na hatia, alimuuwa shahidi kiongozi mkuu wa Mashia bali hata wa Waislamu, ambaye alikuwa akionesha mapenzi kwa Wakristo, kwa ushirikiano na genge la kihalifu la utawala wa Kizayuni siku 40 zilizopita.
Hatua hii si tu tishio dhidi ya mfumo wa Kiislamu wa Iran, bali pia ni matusi ya wazi dhidi ya dini zote za Ibrahimu.
Mitume wote waliwakataza wafuasi wao kuwatusi viongozi wa dini nyingine, na mafundisho ya Mtume wetu yanalaani aina yoyote ya kukosa adabu na matusi dhidi ya viongozi wa dini; lakini kwa masikitiko, rais mhalifu wa Marekani safari hii amekutusi wazi mara kadhaa wewe kama kiongozi wa Wakristo duniani.
Mimi ninalaani kwa nguvu zote hatua hii, na ninatoa tahadhari kwa wafuasi wote wa Nabii Isa (as), bali hata dini zote za Ibrahimu, kwamba iwapo hatutasimama dhidi ya kiburi, udikteta na majivuno ya Firauni wa zama hizi, basi tunapaswa kutarajia matusi na hatari zaidi. Katika jambo hili, Waislamu, Wakristo na Wayahudi wa Marekani wana jukumu kubwa zaidi.
Dini za Ibrahimu, hususan wanazuoni wa Kikristo na Kiislamu, wanaweza kwa kushirikiana kuchukua hatua za kielimu na kivitendo zenye athari kubwa katika kufanikisha lengo lao la pamoja, nalo ni kueneza amani duniani na kuwatetea waliodhulumiwa na wanyonge.
Mwisho, ninatamani kwamba; kwa kudhihiri kwa Mwokozi wa mwisho—ambaye Nabii Isa (as) pia atadhihiri pamoja naye—haki isambae duniani kote na dhulma pamoja na madhalimu vitoweke kabisa. InshaAllah.
Mahmoud Rajabi
Rais wa Taasisi ya Elimu na Utafiti ya Imam Khomeini (rh)
Maoni yako